Saturday, October 28, 2023

KIKOSI CHA SIMBA KILICHOPANGWA KUIANGUSHA AL AHLY CHAHAMISHIWA KWA MBABE WA YANGA IHEFU

MOSSES PHIRI APEWA RUNGU KUWAUA WAKULIMA WA MPUNGA

Mshambuliajii Moses Phiri leo ana nafasi kubwa ya kuanza kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 1 usiku Jana katika Mkutano na Wanahabari, Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira alidokeza kuwa kuna wachezaji leo atawapa nafasi ya kuanza. Phiri ni miongoni mwa wachezaji ambao pasipo na shaka, anaweza kutumika kwenye mchezo huo Ukiacha maoni ya Wanasimba na wale wanaohoji kwa nini Phiri hapewi dakika nyingi za kucheza, katika dakika hizo chache, Phiri ameonyesha kuwa na ufanisi kuliko hata wale wanaoanza Mijadala imekuwa mingi, leo huenda Wanamsimbazi wakafurahi kwa kumuona Mzambia huyo akianza. Wachezaji wengine ambao wanaweza kutumika leo ni pamoja na Luis Miquissone na Shabani Iddi Chilunda ambaye amekuwa akifanya vizuri katika mechi za kirafiki **************

MBABE WA YANGA AANDALIWA DOZI YA USINGIZI NA MSHIRIKI WA AFL

Baada ya kikosi cha Simba kurejea kutoka Misri, Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally alisema nguvu zote zinahamishiwa kwenye mechi zinazofuata katika ligi kuu ya NBC Mchezo dhidi ya Ihefu Fc ndio unaofuata kwenye ratiba ambapo Jumamosi, Oktoba 28 Simba itashuka uwanja wa Mkapa kumenyana na walima mpunga hao kutoka Mbarali Ahmed amesema mkakati wa Simba ni kuendelea kugawa vipigo kwa kila timu inayokuja mbele yao. Ahmed amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa Jumamosi katika mchezo huo ambao wamedhamiria kutoa adhabu kali kwa ihefu FC "Sasa focus ni kwenye ligi kuu ya NBC, Tuendelee kugawa dozi kila anaekuja mbele yetu Wana Lunyasi tuanze sasa kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Wababe wao Jumamosi ya October 28 Benjamini Mkapa," alitamba Ahmed Baada ya mchezo huo, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Yanga, utapigwa Novemba 05 katika uwanja wa Benjamin Mkapa. Pengine huu ndio mchezo ambao mashabiki wa Simba wanausubiri kwa hamu, alama tatu katika mchezo huu zitaendelea kupalilia safari ya ubingwa msimu huu

MKUDE AMGEUKA MO AMDAI FIDIA YA BIL MOJA

Kiungo wa Yanga SC, Jonas Mkude amefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiidai Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) fidia ya Tsh bilioni moja kwa kutumia picha zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na X (zamani Twitter) bila idhini yake. Mkude ambaye alijiunga na Yanga baada ya kuondoka Simba amefungua kesi ya madai 192 ya mwaka 2023 mbele ya Jaji Butamo Philip dhidi ya kampuni hiyo akidai fidia hiyo Kwa kuvunja haki yake ya msingi.
< A midfielder of Young SC, Jonas Mkude has opened a case in the High Court in the Dar es Salaam region demanding compensation of one billion Tsh from Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) for using his photos in various social networks including Instagram and X (formerly Twitter) without his approval. Mkude, who joined Yanga after leaving Simba, has filed a 192 claim case of 2023 before Judge Butamo Philip against the company claiming compensation for violating his basic right.

Wednesday, October 25, 2023

KOCHA GAMONDI ACHUKIZWA NA TABIA ZA METACHA AMUENGUA

Kipa Namba Mbili wa Yanga, Metacha Mnata ameshakitibua tena pale Yanga na sasa amewekwa kando na kikosi hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu. . Inaelezwa kipa huyo ameingia kwenye utata wa Utovu wa nidhamu na Kocha Gamondi baada ya kushindwa kurejea kambini kwa wakati. . Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kwamba Metacha hakufanya mawasiliano yoyote akiwa nje ya kikosi hicho. Mbali na Metacha inaelezwa pia kiungo Jonas Mkude, naye mapema alifanya kosa kama hilo ingawa aliwahi na kujisalimisha na kupewa adhabu za ndani na baadaye kusamehewa. Ingawa chanzo hicho cha Uhakika hakikueleza ni Metacha amewekwa pembeni kwa muda gani Hii ni Hot water blogspot.com

BAADHI YA MASHABIKI WA YANGA WAMTAKA GAMONDI KUMUIGA ROBERTINOH ILI KUONDOAFEDHEHA KWA AL AHYL KWENYE MAKUNDI

USHIRIKI wa Timu ya soka ya Simba sports club ya Tanzania katika mashindano ya ligi kubwa mpya uliozishirikisha timu bora Nane Barani Afrikadhidi ya Al Ahly ya Misri kumetoa funzo kwa kocha wa timu ya klabu ya Young Africans Muargentina Miguel Gamondi kujifunza mkakati wa kuikabili dhidi ya timu ya Al Ahly iliyocheza dhidi ya Simba iliyoshirki mashindano hayo ya AFL kwa ajili ya kupata ushindi katika ligi ya vilabu bingwa afrika inayotarajiwa kuanza Nov 24 2023. Gamondi pia alikririwa akieleza kuwa atakuwa makini katika mchezo wa awali kuifuatilia kufahamu mfumo na mbinu na aina ya wachezaji kwa ajili ya maandalizi na Al Ahly aidha pia kumfuatilia kocha Robertinoh mbinu na mfumo waaliyoitumia kwa ajili ya maangamizi., ”Ni kweli endapo Gamondi hatamuiga Robertinoh basi tutakufa mbele yao lakini anapaswa kumtafuta Robertinoh ili amsaidie yanga kama huu ulio sahihi na Simba wamefuta Uteja tofauti na matarajio yetu tumebaki sisi,,,,,,,,,,,aliongea hamisi bakari shabiki wa yanga Hamisi anasisitiza kumtaka Gamondi kutumia mfumo wa Robertinoh huku akitofautisha mashindano ya CL yanayohitaji pointi nay ale ya APL yanayozingatia idadi kubwa ya magoli Huku akisema Simba imefungua darasa ambalo Yanga wanatakiwa kuiga

FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE

Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...