Friday, November 17, 2023
SABAYA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA YA RUFAA
Mahakama ya Rufaa imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Kilimanjaro Lengai ole Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura baada ya mahakama hiyo kukubaliana na maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha,
Rufaa hiyo namba 231 ya mwaka 2022 ilikatwa na mwendesha mashtaka wa serikali (DPP) kupinga uamuzi wa awali wa hukumu ya rufaa namba 129 ya mwaka 2021 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mbele ya Jaji Sedekia Kisanya iliyompa ushindi Sabaya na wenzake baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kufuatia kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021 iliyohusisha wizi na makundi ya unyang’ayi wa kutumia silaha.
BODI YA WAKURUGENZI YA SIMBA YATANGAZA KUWAACHA WACHEZAJI
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ ameweka wazi kuwa wachezaji ambao hawataonyesha uwezo wao na kujituma uwanjani hawatuvumiliwa hivyo wataachwa.
Try Again amesema katika kipindi cha mwezi mmoja na siku chache kilichobaki kuelekea dirisha dogo la usajili kila mchezaji anapaswa kujituma na kuonyesha uwezo wake la sivyo ataachwa.
Try Again ameongeza kuwa Simba haiwezi kuwa na wachezaji ambao wanalipwa kiasi kikubwa cha pesa na bado wanakaa benchi kutokana viwango kushuka.
“Baada ya matokeo tuliyopata siku za karibuni tumefanya tathimini ili kuona tumekwa wapi na tumegundua wachezaji wengi hawajitumi. Tumewaambia hatuta wavumilia kila mmoja anapaswa kujituma,” amesema Try Again.
Akizungumzia dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa mwezi ujao Try Again amesema “tutasajili lakini kwa mapendekezo ya mwalimu mpya ambaye tutamtangaza karibuni.
“Unajua unaweza kumsajili mchezaji hata kutoka Al Ahly lakini akaja hapa na kocha asimtumie, tutampa jukumu hilo yeye kwakuwa ndiye anajua anataka mchezaji wa aina gani kwenye kikosi chake,” amesema Try Again.
AMROCHE WACHEZAJI WENGI WA TIMU YA TAIFA WANAKAA BENCHI KWENYE VILABU VYAO.
“Cha kusikitisha tuna wachezaji wengi ambao hawachezi katika vilabu vyao. Klabu hazitusaidii sana kwa sababu tunawezaje kuwa na timu nzuri ya taifa ikiwa wachezaji wazuri wa timu ya taifa wanakaa benchi."-Adel Amrouche, Kocha wa Taifa Stars.
Subscribe to:
Comments (Atom)
FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE
Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...
-
MAKAMU wa Rais Dr Mohamedi Ghalib Bilal leo majira ya saa ya saa 7 mchana anatarajia kufungua chuo cha ufundi stadi mjini Babati mkoani M...







