Monday, November 20, 2023
FIFA KUMWAGA MAHELA KWA WACHEZAJI MAJERUHI
🚨FIFA italazimika kuilipa Barcelona fidia ya euro 20,548 kwa kila siku ambayo Gavi atakuwa nje ya uwanja tangu alipoumia akiwa kwenye majukumu ya kimataifa. malipo yataanza siku 28 baada ya mchezaji huyo kupata jeraha na yanaweza kudumu kwa muda usiozidi mwaka mmoja.
Hii ni taratibu ya FIFA ikitokea Mchezaji anapata Majeraha akiwa anatimiza Majukumu katika timu yake ya Taifa basi Shirikisho la Mpira Ulimwenguni yaani FIFA litatoa fidia kwa Mchezaji huyo.
Source [@mundodeportivo]
YANGA KABLA YA KUEPA KUKUTANA NA CRBELOUZIDAD INA JAMBO LAO
🟡Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu ya Yanga itasafiri Jumatatu hii November 20, 2023 kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi klabu bingwa Afrika.
🟡Pia Yanga siku ya Jumatatu hii watazindua Jezi za michuano ya klabu bingwa Afrika, ambapo watazindua jezi mapema na Usiku wataanza safari ya kuelekea Algeria.
Inatajwa maudhui ya goli tano alizopasuka Simba dhidi ya Yanga zitawekwa kwenye Jezi hiyo, NIMETHIBITISHA.
MPAMBANO WA KOMBE LA DUNIA JE WATANZANIA WATATOBOA?
Baada ya kupata ushindi mchezo uliopita, Taifa Stars kesho Jumanne watakuwa dimba la Benjamin Mkapa wakikipiga na Morocco kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia
Mechi hii itaruka mbashara kupitia#ZBC2 kuanzia saa 4:00 usiku.
#TaifaStars #WorldCup2026 #Morocco
Subscribe to:
Comments (Atom)
FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE
Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...
-
MAKAMU wa Rais Dr Mohamedi Ghalib Bilal leo majira ya saa ya saa 7 mchana anatarajia kufungua chuo cha ufundi stadi mjini Babati mkoani M...


