Saturday, October 28, 2023

MBABE WA YANGA AANDALIWA DOZI YA USINGIZI NA MSHIRIKI WA AFL

Baada ya kikosi cha Simba kurejea kutoka Misri, Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally alisema nguvu zote zinahamishiwa kwenye mechi zinazofuata katika ligi kuu ya NBC Mchezo dhidi ya Ihefu Fc ndio unaofuata kwenye ratiba ambapo Jumamosi, Oktoba 28 Simba itashuka uwanja wa Mkapa kumenyana na walima mpunga hao kutoka Mbarali Ahmed amesema mkakati wa Simba ni kuendelea kugawa vipigo kwa kila timu inayokuja mbele yao. Ahmed amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa Jumamosi katika mchezo huo ambao wamedhamiria kutoa adhabu kali kwa ihefu FC "Sasa focus ni kwenye ligi kuu ya NBC, Tuendelee kugawa dozi kila anaekuja mbele yetu Wana Lunyasi tuanze sasa kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Wababe wao Jumamosi ya October 28 Benjamini Mkapa," alitamba Ahmed Baada ya mchezo huo, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Yanga, utapigwa Novemba 05 katika uwanja wa Benjamin Mkapa. Pengine huu ndio mchezo ambao mashabiki wa Simba wanausubiri kwa hamu, alama tatu katika mchezo huu zitaendelea kupalilia safari ya ubingwa msimu huu

No comments:

FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE

Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...