Monday, October 30, 2023

MO DEWJI AUNDA BARAZA LA USHNDI KLABU BINGWA YA AFRIKA NA UBINGWA LIGI YA NBC

Rais wa heshima wa klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ amefanya uteuzi wa wajumbe 21 wa Baraza la Ushauri wa klabu kwa ajili ya maendeleo. Moja ya majukumu ya Raisi wa heshima ni kuhakikisha Uongozi na Utawala bora unazidi kuboreshwa kila wakati ili kuzidi kusukuma gurudumu la maendeleo ya klabu. Baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Mo amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Ushauri ( Advisory Board) wa klabu. 1. Jaji Thomas Mihayo M/kiti 2. Hassan Dalali-Mjumbe 3. Ismail Aden Rage-Mjumbe 4. Evans Aveva-Mjumbe 5. Faroukh Baghoza 6. Swedi Nkwabi-Mjumbe 7. Azim Dewji-Mjumbe 8. Kassim Dewji-Mjumbe 9. Musleh Al-Ruweh-Mjumbe 10. Mohamed Nassor-Mjumbe 11. Mulamu Ng’ambi-Mjumbe 12. Octavian Mshiu-Mjumbe 13. Prof Mohamed Janabi-Mjumbe 14. Hassan Kipusi-Mjumbe 15. Geofrey Nyange-Mjumbe 16. Gerald Yambi-Mjumbe 17. Moses Kaluwa-Mjumbe 18.Crescentius Magori-Mjumbe 19. Juma Pinto- Mjumbe 20. Mwina Kaduguda-Mjumbe 21. Idd Kajuna-Mjumbe Kazi kubwa ya Baraza hili itakuwa ni kuishauri Bodi juu ya maendeleo ya klabu Uongozi na Utawala bora.

MKURUGENZI WA SHERIA WA YANGA AMLILIA SHABIKI WAO ALIYEADABISHWA KWA KIPIGO DHIDI YA MASHABIKI WA MNYAMA

Mkurugenzi wa sheria wa Yanga amesema kesho klabu ya Yanga itawasilisha rasmi malalamiko yake kwenye mamlaka juu ya kitendo cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga jana kwa Mkapa. "Mpira ni upendo, kwa kitendo hiki cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga kiasi hiki sio utu kabisa, hakuna sababu ya msingi kumshambulia mtu kiasi hiki. Labda niwakumbushe washamba wote walioshiriki unyama huu, Yanga na Simba ni Watani wa jadi sio maadui" "Isije kufika siku hatuwezi kukaa kwa pamoja kama ndugu kwa sababu ya UPUMBAVU kama huu. Naiomba bodi ya ligi @tplboard, TFF @tanfootball na Polisi @policetanzania wachunguze suala hili na hatua kali zichukuliwe" "Klabu itawasilisha malalamiko yake rasmi kesho na tutaomba hatua kali zichukuliwe kwa huu unyama.. Shame on you all who're involved in this incident" "Mwenye kumjua na kuwa na mawasiliano ya huyu (Shabiki wa Yanga aliyepigwa na mashabiki wa Simba) anitumie tafadhali" Licha ya Mkurugenzi huyo kulaani tukio hilo lakini baadhi ya wadau wa Soka wamemshauri kabla ya kutoa tamko alitakiwa kutambua Kiini cha kupigwa dhidi y mashabiki wa timu hiyo ambao hawana historia ya matukio kama hayo tofauti na mashabiki wa Yanga ambao walishamchania mshabiki wa soka Moshi na kuichoma moto.lakini pia mji kasoro bahari Morogoro sambamba na kumpiga shabiki wa Coastal Union jijini Arusha baada kumalizika kwa mikwaju kwenye fainali za FA

AMINI USIAMINI HUYU NI SARAFINA MWIGZAJI MAARUFU ALIETIKISA BONGO

Picha mbili tofauti (zamani na sasa) za Leleti Khumalo mwigizaji toka Afrika Kusini, alizaliwa tarehe 30 Machi 1970 kwa sasa ana umri wa miaka 53. Wengi tunamfahamu kwa jina la Sarafina kutokana na movie maarufu aliyoshiriki ya enzi za ubaguzi wa rangi iliyoitwa SARAFINA! Unakumbuka nini kuhusiana na movie ya Sarafina? Mimi kuna baadhi ya matukio yalinitoa machozi na kunifanya niwachukie sana wabaguzi wote wa rangi
Two different photos (past and present) of Leleti Khumalo, an actress from South Africa, she was born on March 30, 1970 and is currently 53 years old. What do you remember about Sarafina's movie? There are some events that brought tears to my eyes and made me hate all the racists

FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE

Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...