Saturday, December 2, 2023

AZAM YAMTOLEA SHIJA UCHOVU YAMBANA KOROMEO

TAARIFA KWA UMMA Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigizaji na mtengeneza filamu, Deogratius Shija, akiwatuhunu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yetu kwa vitendo vya rushwa. Kampuni yetu inamuarifu Shija na umma kwa ujumla kuwa, haivumilii vitendo vya rushwa, udanganyifu na mbinu zozote chafu katika kusaili maudhui kwa ajili ya kuonyeshwa katika chaneli zetu, kadhalika hatupendezwi na tabia ya watengeneza maudhui kutunga shutuma dhidi ya watendaji wetu kwa sababu tu kazi zao hazikupitia kwenye chujio la kupima ubora. Kwasababu hizo, tunatoa muda wa wiki mbili kwa Deogratias Shija, kuwasilisha ushahidi au vielelezo kuhusu tuhuma alizozitoa kwa Mkurugenzi Mtendaji au kwenye mamlaka za kisheria, TAKUKURU, Film Board, au Jeshi la Polisi, ili kuwezesha hatua stahiki zichukuliwe kwa watuhumiwa wote wanaodaiwa kuihujumu kampuni kwa vitendo vyote kinyume na taratibu za kazi. Kampuni yetu ina utaratibu maalum wa ndani, ulio wazi na shirikishi katika manunuzi ya filamu na maudhui mengine kutoka kwa wazalishaji binafsi. Azam Media Ltd inatumia fursa hii kuwaomba wadau wa filamu nchini kufuata njia sahihi zinazokubalika kisheria ikiwemo kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji, Bodi ya Filamu, Polisi au TAKUKURU pale wanapokuwa na ushahidi wa madai yao badala ya kutumia njia ambazo zinaweza kuleta taharuki na taswira mbaya kwa jamii ndani na nje ya Tanzania. Imetolewa na Idara ya Mawasiliano kwa Umma 1.12.2023

GAMONDI AMPONDA ALI KAMWE

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, ameeleza kutokubaliana na utaratibu wa kuita mchezaji jina la mchezo, akisisitiza umuhimu wa kuangazia timu nzima akisema “Sikubaliani kabisa na huu utaratibu wa kuita mchezo jina la mchezaji, kwa sababu mchezaji hayupo peke yake wapo timu. Jambo muhimu kwangu ni timu sio mchezaji mmoja, ila naelewa ndio utaratibu wa timu kwa ajili ya kufanya marketing, kuwafanya mashabiki waje uwanjani na kuuelewa zaidi mchezo husika, najua huo ndio utara… See more

FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE

Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...