Tuesday, May 1, 2012

MAKAMU WA RAIS DR BILALI AKITEMA CHE CHE BABATI

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania dr Mohamedi Ghalib Bilal amesema umefika wakati kwa serikali kusimamia kidete suala la kuimarisha na kukuza elimu ya ufundi stadi ili kuwajengea uwezo watanzania waweze kukabiliana na soko la ushindani la jumuiya ya afrika ya mashariki ambapo wajasiriamali wameanza kuingia nchini hali ambayo kama serikali italala upo uwezekano watanzania wakawa hawana uamuzi katika kukuza uchumi wao
akihutubia umati mkubwa wa wananchi mjini babati baada ya kuzindua na kutembelea chuo cha VETA amesema umefika wakati kwa serikali kutoa msukumo kwa jamii kujiunga na VETA ili kuleta tija kabla ya sko hilo halijavamiwa na wananchi jirani na Tanzania.
"elimu ya ufundi ni kichocheo cha ajira za mapema kabla ya kukamilika kwa jumuiya ya afrika ya mashariki,lakini idadi ya wanaohitimu ni ndogo mfano takwimu zinaonyesha kuwa 2006 uwiano wa fundi mchundo na mwananchi ni kati ya fundi mmoja 1:1618 halii inatisha kama watanzania wasipoliangalia kwa makini"
Hata hivyo ameitaka serikali kujizatiti kuhakikisha kuwa elimu ya ufundi stadi inakua ili kuongeza pato la uchumi na watanzania wakiwa wanaongoza katika ajira badala ya wageni toka nje ya nchi.
Nae balozi wa Korea ya kusini bw Young Hoon kim amesema serikali yake itahakikisha inaisaidia serikali ya Tanzania ili iweze kupata wataalamu wa teknolojia ya ufundi standi inasimama'
mwisho










Hii ni ngoma ya jamii ya kabila la wairaq la wagorowa wakifanya vitu vyao baada ya makamu Rais kuwasili kabla ya kuzindua VETA Babati-hawa jamaa ni hatari wasiponyamazishwa ama kufukuzwa eneo la tukio hucheza hata siku tano huku wakiwaalika wenzao jambo ambalo limeonekana kwa maambukizi ya ukimwi ni hatari

MAKAMU Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr Mohamedi Ghalib Bilal akiwasili kwenye eneo la chuo cha Ufundi stadi VETA kilichopo mjini Babati mkoa wa Manyara anaonekana akisalimiana na timu ya wakuu wa wilaya tano za mkoa wa Manyara dakika chache kabla ya kuzindua chu hicho kilichopo eneo la Waang'waray mjini babati leo Aprili 30 mwaka huu-picha na mwandishi wetu wa water pwaa!! pwaa!! pwaa!

Monday, April 30, 2012

Dr BILAL MAKAMU RAIS TANZANIA NDANI YA BABATI VETA


MAKAMU wa Rais Dr Mohamedi Ghalib Bilal leo majira ya saa ya saa 7 mchana anatarajia kufungua chuo cha ufundi stadi mjini Babati mkoani Manyara muda mchache baada ya kuwasili kwenye eneo la chuo hicho kilichopo eneo la Wang’waray.
Lengo la kufunguliwa kwa chuo hicho ni kusogeza elimu ya ufundi stadi kwa wakazi wa mkoa huo kwa wahunzi na wengineo  hususani vijana ambao wengi wao watapata uwezo wa kujiajiri wenyewe kupitia fani mbalimbali zilizoanza kutolewa tangu kilipoanza kupokea wanafunzi wapya mwezi Januari mwaka huu.
Aidha kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Manyara Bw Elaston John Mbwillo amesema dr Bilali kabla ya kuzindua chuo hicho na kupokelewa na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi bw Shukuru Kawambwa kwa ushirikiano na mkuu wa mkoa huo atapanda atapanda mti wa kumbukumbu pamoja na balozi wa Korea kusini walioshirikiana kujenga chuo hicho.
Burudani kedekede zitaburudishwa kwenye eneo la chuo hicho ili kusherehesha sherehe hizo za ufunguzi kabla ya mkuu wa VETA kumkaribisha mkuu wa mkoa na hatimaye waziri Kawambwa ambaye atamkaribisha Dr Ghalib kueleza ujumbe kwa wananchi.
Baadhi ya wananchi wameiambia glob ya water pwaa!! Pwaa!! Pwaa! Kuwa kuanzishwa kwa chuo hicho ni faraja lakini pia wataweza kuimarisha fani ya ufundi huo ambayo kwa miaka mingi wamekuwa wakiifanya bila ya ujuzi kamili na kushindwa kuingia katika soko la ushindani la afrika ya mashariki.
Aidha pia wameitaka VETA kuacha longolongo kwa kuchaguana kwani kama watatoa uhuru klwa vijana waliomaliza elimu ya msingi bila shaka wataweza kumsaidia dr JK kukamilisha ndoto zake maisha bora kwa kila mtanzania sanjari na kutoa ajira kwa zile ajira milioni moja hadi kufikia ukomo wa uongozi wake.

Sunday, April 29, 2012

KAMATI KUU YA CCM YABARIKI RAIS JAKAYA KIKWETE KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI



Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.
      Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na  taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;     
 
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza   juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.
   
2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais   KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.
           
Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.
           Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.

Friday, November 19, 2010

18 students are in lock-up in Manyara,breaking news!!

Polisi mkoani Manyara inawashikilia wanafunzi 18 wa shule ya sekondari ya bweni ya Balangdalalu wilayani Hanang mkoani Manyara kutokana na tuhuma za kumshambulia mkuu wa shule hiyo Bw Godlivin Tiaso kwa vitu vyenye ncha kali na mawe na kumsababisia kulazwa kuharibu mali za shule hiyo kutokana na kile kinachodaiwa kumtuhumu kukutwa na mwanafunzi wa kike nyakati za usiku.
akithibitisha kutokea kwa vurugu hizo juzi kamanda wa polisi mkoani Manyara Bw Parmena Sumary akizungumzia tukio hilo (leo Nov 19)amesema polisi imelazimika kuwashikilia wanafunzi hao na kuendelea kuwahoji na wakibainika kuhusika moja kwa moja itawafikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo za uharibifu wa mali pamoja na shambulio.
Aidha kamanda Sumary amesema kabla ya wanafunzi hao kumshambulia mkuu huyo wa shule katika tukio hilo lililotokea usiku wa manane walimwandaa mwanafunzi wa kike wa kidato cha tatu kwenda kumwamsha mkuu huyo bw Tiaso ili kumsikiliza matatizo yake na alipotoka nyumbani kwake ,mwanafunzi huyo alimwita pembeni na kutoa ishara kwa wananfunzi wenzake.
Hata hivyo kamanda Sumary amesema wanafunzi hao walianza kumpiga kwa vitu vigumu na mawe wakimtuhumu kumfumania mwalimu na mwanafunzi huyo tuhuma ambazo amesema polisi inazifanyia kazi na kuharibu mali za shule ambazo gharama yake bado haijafahamika.
Kwa upande mwingine mkuu wa shule hiyo Bw Godliving Tiaso alipoulizwa na radio one kwa njia ya simu toka katika hospitali ya Tumaini ya halmashauri ya wilaya ya Hanang alipolazwa amesema tukio hilo limetokana na ukosefu wa nidhamu ya shule lakini pia hakufumaniwa na mwanafunzi huyo kama wananfunzi hao walivyosambaza uvumi huo.
je, wananchi katika hili mnalziungumziaje?
mwisho

wazee wa nchi

FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE

Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...