MAKAMU wa Rais Dr Mohamedi Ghalib Bilal leo majira ya saa ya
saa 7 mchana anatarajia kufungua chuo cha ufundi stadi mjini Babati mkoani
Manyara muda mchache baada ya kuwasili kwenye eneo la chuo hicho kilichopo eneo
la Wang’waray.
Lengo la kufunguliwa kwa chuo hicho ni kusogeza elimu ya
ufundi stadi kwa wakazi wa mkoa huo kwa wahunzi na wengineo hususani vijana ambao wengi wao
watapata uwezo wa kujiajiri wenyewe kupitia fani mbalimbali zilizoanza kutolewa
tangu kilipoanza kupokea wanafunzi wapya mwezi Januari mwaka huu.
Aidha kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Manyara Bw Elaston John
Mbwillo amesema dr Bilali kabla ya kuzindua chuo hicho na kupokelewa na waziri
wa elimu na mafunzo ya ufundi bw Shukuru Kawambwa kwa ushirikiano na mkuu wa
mkoa huo atapanda atapanda mti wa kumbukumbu pamoja na balozi wa Korea kusini
walioshirikiana kujenga chuo hicho.
Burudani kedekede zitaburudishwa kwenye eneo la chuo hicho
ili kusherehesha sherehe hizo za ufunguzi kabla ya mkuu wa VETA kumkaribisha
mkuu wa mkoa na hatimaye waziri Kawambwa ambaye atamkaribisha Dr Ghalib kueleza
ujumbe kwa wananchi.
Baadhi ya wananchi wameiambia glob ya water pwaa!! Pwaa!! Pwaa!
Kuwa kuanzishwa kwa chuo hicho ni faraja lakini pia wataweza kuimarisha fani ya
ufundi huo ambayo kwa miaka mingi wamekuwa wakiifanya bila ya ujuzi kamili na kushindwa
kuingia katika soko la ushindani la afrika ya mashariki.
Aidha pia wameitaka VETA kuacha longolongo kwa kuchaguana
kwani kama watatoa uhuru klwa vijana waliomaliza elimu ya msingi bila shaka
wataweza kumsaidia dr JK kukamilisha ndoto zake maisha bora kwa kila mtanzania
sanjari na kutoa ajira kwa zile ajira milioni moja hadi kufikia ukomo wa
uongozi wake.
No comments:
Post a Comment