Friday, November 17, 2023

BODI YA WAKURUGENZI YA SIMBA YATANGAZA KUWAACHA WACHEZAJI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ ameweka wazi kuwa wachezaji ambao hawataonyesha uwezo wao na kujituma uwanjani hawatuvumiliwa hivyo wataachwa. Try Again amesema katika kipindi cha mwezi mmoja na siku chache kilichobaki kuelekea dirisha dogo la usajili kila mchezaji anapaswa kujituma na kuonyesha uwezo wake la sivyo ataachwa. Try Again ameongeza kuwa Simba haiwezi kuwa na wachezaji ambao wanalipwa kiasi kikubwa cha pesa na bado wanakaa benchi kutokana viwango kushuka. “Baada ya matokeo tuliyopata siku za karibuni tumefanya tathimini ili kuona tumekwa wapi na tumegundua wachezaji wengi hawajitumi. Tumewaambia hatuta wavumilia kila mmoja anapaswa kujituma,” amesema Try Again. Akizungumzia dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa mwezi ujao Try Again amesema “tutasajili lakini kwa mapendekezo ya mwalimu mpya ambaye tutamtangaza karibuni. “Unajua unaweza kumsajili mchezaji hata kutoka Al Ahly lakini akaja hapa na kocha asimtumie, tutampa jukumu hilo yeye kwakuwa ndiye anajua anataka mchezaji wa aina gani kwenye kikosi chake,” amesema Try Again.

AMROCHE WACHEZAJI WENGI WA TIMU YA TAIFA WANAKAA BENCHI KWENYE VILABU VYAO.

“Cha kusikitisha tuna wachezaji wengi ambao hawachezi katika vilabu vyao. Klabu hazitusaidii sana kwa sababu tunawezaje kuwa na timu nzuri ya taifa ikiwa wachezaji wazuri wa timu ya taifa wanakaa benchi."-Adel Amrouche, Kocha wa Taifa Stars.

Diamond amtambulisha msanii Mpya wasafi....

AZAM KUUMANA NA GOR MAHIA

RATIBA YA TAIFA STARS

Thursday, November 16, 2023

DAR YOUNG YAPANIA KUVURUGA AS VITA

Kwa mujibu wa chanzo changu ni kuwa Klabu ya Yanga imefungua mazungumzo rasmi na Uongozi wa klabu ya AS Vita Club ili kununua mkataba wa Elie Mpanzu ambaye ni winga wa kulia. - Winga Elie Mpanzu amebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja katika Klabu ya AS Vita, na Mchezaji ameshawishika kujiunga na Klabu ya Yanga dirisha lijalo la uhamisho. - Baada ya Uongozi wa Yanga kupokea ripoti ya mapendekezo ya usajili kutoka kwa Kocha mkuu Miguel Gamondi, Uongozi umeanza kuyafanyia kazi mahitaji ya mwalimu mapema. - Klabu ya Yanga inapambana sana kukamilisha dili hilo kwa wakati.

Tuesday, November 14, 2023

MALARIA NCHINI HAITMALIZIKA IKIWA MBU HAWA HAWATAANGAMIZWA

Takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya ugonjwa wa malaria nchini bado ni changamoto licha ya kuendelea kupungua kutoka asilimia 14.7 mwaka 2015 hadi sasa kufikia asilimia 8.1 huku mikoa mitano ikiongoza kanda ya ziwa na Mtwara ambayo maambukizi yapo juu ya asilimia 8 Je, nini kifanyike ili ugonjwa wa malaria utokomee kabisa nchini? Tumia lugha ya staha kwenye kutoa maoni yako.

FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE

Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...