Wednesday, November 8, 2023
THUBUTU MANGUNGU AAPA HAJIUZULU UENYEKITI KLABU YA SIMBA
🗣"Nijiuzulu kwa sababu gani, kwani timu inafanya vibaya ? Tumepoteza mechi 1 tu, kwa nini hawakusema nijiuzulu wakati tunashinda mfululizo?"
WANA NGUVU MOJA MMESIKIA MANGUNGU ?
Baadhi ya wadau wa soka wakizungumzia shinikizo la kutakiwa kujiuzulu lililozagaa mitandaoni wanasema hao wanamtaka Mangungu ajiuzulu wanapata shinikizo nyuma ya nani??? tatizo halionekani na je hao wanamtaka ajiuzulu sio waliomchagua yeye kuwa mwenyekiti?
MANULA NA BOCCO WAITWA TIMU YA TAIFA KULIPIGANIA TAIFA BADO BOCCO ATABAKIA KUWA BOCCO
Nyota wetu wanne wameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kitakachoingia kambini kujiandaa na mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia.
Nyota hao ni mlinda mlango, Aishi Manula kiungo mkabaji, Mzamiru Yassin na washambuliaji John Bocco na Kibu Denis.
Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya nyama za paja Manula amerejea katika kikosi cha Stars.
Stars itacheza mechi mbili za kufuzu dhidi ya Niger na Morocco.
Wapo mashabiki wengi nchini wanamtusi Bocco lakini hao ni kutokana na kutokuwa na weledi wa mchezo wa soka,Bado Bocco ni mchezaji mwenye kiwango cha kuendelea kuthaminiwa na Taifa kwa kuwa anao uwezo na mpaka sasa hakuna mchezaji yeote mshambuliaji kama Bocco wengine ni ushabiki lakini bado Caputano John Raphael Bocco anastahili kupewa maua yake
MIGUEL KOCHA WA YOUNG AFRICANS HANA NENO DHIDI YA MCHEZO NA COASTAL UNION
"Sina mengi ya kuzungumza kuelekea mchezo wetu wa leo Nov 9 2023 dhidi ya Coastal Union kwasababu ya muda, jana tumetumia siku yetu kwa ajili ya kurudisha miili sawa na kusafiri kuja Tanga. Na leo tutakuwa na mazoezi kidogo jioni hayo ndio ninayoweza kusema kwa sasa" Gamondi
Subscribe to:
Comments (Atom)
FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE
Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...
-
TAARIFA KWA UMMA Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigiz...
-
🟡Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu ya Yanga itasafiri Jumatatu hii November 20, 2023 kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza...






