Friday, November 3, 2023

TFF KUWASHUGHULIKIA WALIOMDUNDA SHABIKI ALIYEVAA JEZI YA YANGA

Bodi ya Ligi Kuu pia imeelezwa kusikitishwa na kitendo cha ukatili na vurugu kilichofanywa na mashabiki waliokuwa wamevaa jezi ya Simba na bluu kumshambukia shabiki wa Yanga katika mechi ya Simba vs Ihefu Uwanja wa Mkapa. Bodi ya Ligi Kuu pia imeelezwa kusikitishwa na kitendo cha ukatili na vurugu kilichofanywa na mashabiki waliokuwa wamevaa jezi ya Simba na bluu kumshambukia shabiki wa Yanga katika mechi ya Simba vs Ihefu Uwanja wa Mkapa. “Bodi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama inakamilisha mchakato wa kuwatambua mashabiki wote waliohusika na tukio hilo kabla ya kuwachukulia hatua kali,” imeeleza taarifa hiyo.

GAMONDI ATUMIA DAKIKA 180 KUMSOMA MNYAMA ILI KUEPUKA KUKANDWA

Ni Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amewasoma wapinzani wao Simba kwa muda wa dakika 180 baada ya kuwachambua wapinzani wake.Novemba 5 Yanga wanatarajiwa kuwa wageni wa Simba kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Uwanja wa Mkapa. Yanga imekusanya pointi 18 baada ya kucheza mechi saba huku Simba pia wakiwa na pointi 18 baada ya kucheza michezo sita. Gamondi alitumia dakika 90 za kwanza za mchezo wa robo fainali ya AFL ambapo alitua kwa Mkapa kutazama mchezo huo ambao ulimalizika kwa Simba kutoa sare ya mabao 2-2. Mchezo mwingine ambao Gamondi aliweza kuushuhudia ulikuwa ni ule wa dhidi ya Ihefu wa ligi kuu ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Kocha Gamondi atakuwa na kazi moja tu ya kuhakikisha kuwa anaipa ushindi yanga mara baada ya msimu uliopita Yanga kupoteza kwa idadi ya mabao 2-0 dhidi ya Simba kocha akiwa ni Nassredine Nabi. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Simba amesema kuwa wanatambua kwamba kocha wa Yanga alikuwa akiwafuatilia hivyo hawana mashaka.

CAF YAUKATAA UWANJA HUKO GHANA

CAF has rejected the Cape Coast Stadium as venue to host Medeama SC's CAFCL group stage matches. Meanwhile, πŸ’° Ghana πŸ‡¬πŸ‡­ received $9million from the 2022 World Cup, the money was shared by the FA officials and players. No one thought about investing some of the money to develop and maintain football facilities. 🏟 This is the state of their best stadium in the country. This venue was closed for renovation a few months ago. NB// If you go to most stadiums in Ghana and want to use the washroom, you have to go home and then come back and continue watching the game. How are countries like Morocco, South Africa, and Algeria able to have multiple quality playing surfaces and facilities and yet other cannot even own just one? πŸ€” Ghana why? πŸ˜‚πŸ˜‚
AF imeukataa Uwanja wa Cape Coast kuwa uwanja wa kukaribisha Medeama SC ya hatua ya makundi ya CAFCL. Wakati huo huo, πŸ’° Ghana πŸ‡¬πŸ‡­ ilipokea dola milioni 9 kutoka kwa Kombe la Dunia la 2022, pesa hizo ziligawanywa na maafisa wa FA na wachezaji. Hakuna aliyefikiria kuwekeza baadhi ya pesa kuendeleza na kudumisha vifaa vya soka. 🏟 Hii ndio hali ya uwanja wao bora zaidi nchini. Ukumbi huu ulifungwa kwa ukarabati miezi michache iliyopita. NB// Ukienda kwenye viwanja vingi vya Ghana na kutaka kutumia chumba cha kuosha, lazima urudi nyumbani kisha urudi na kuendelea kutazama mchezo. Je, nchi kama Morocco, Afrika Kusini, na Algeria zinawezaje kuwa na sehemu nyingi za kuchezea zenye ubora na bado nyingine haziwezi hata kumiliki moja tu? πŸ€” Ghana kwanini? πŸ˜‚πŸ˜‚

Thursday, November 2, 2023

AHMED ALLY ULIMI UTAKUPONZA SHAURI YAKO JIRANI YAKO ANAKUJA KIMYAKIMYA NA MKUKI WENYE SUMU

"Azam hawezi kutufikia tena, mpinzani aliyebaki ni Yanga ambaye na yeye tunataka kumfunga na kumpita kwa alama sita. Ni mechi ambayo tunaitaka kweli kweli, kuanzia kwa mashabiki, benchi la ufundi, wachezaji na viongozi ndio hata hatulali." "Tumewekeza zaidi kwenye kuwafurahisha mashabiki wetu, Jumapili ya Novemba 5, 2023 tunataka kuwafurahisha. Na anayeshinda mchezo huo ndio atatawala nchi hadi tukikutana tena." "Mashabiki wetu tuzingatie misingi ya uungwana na ustaarabu, tujitahidi tushangilia na kutaniana kwa heshima ili kuepusha vurugu. Tuendeleze Utanzania kwa utu na upendo." "Tumecheza mechi ngumu lakini mechi ya Jumapili ni ngumu kuliko zote hii ni kutokana na utani uliopo pamoja na ubora wa timu yao. Tunaona namna wachezaji wao wanajituma. Mechi yetu dhidi yao ni ngumu kweli kweli, mechi ya kipimo cha mpira wa nchi haiwezi kuwa nyepesi."- Ahmed Ally.

KLABU YA SIMBA YAKIA NA SHABIKI WA YANGA KWA MKAPA

REMA WA NIGERIA ATUHUMIWA KUSHIRIKIANA NA MASHETANI KUIMBA MUSIC

Msanii Rema kutoka nchini Nigeria amekutana na tuhuma za Mashabiki Kwenye Mitandao ya Kijamii zikidai kuwa Msanii huyo anajihusisha na imani za kishetani na hii ni baada ya kuachia Video clip ya wimbo wake mpya wa smooth Criminal ambao upo kwenye Ep yake Mpya ya Ravage inayo tarajiwa kutoka siku ya ijumaa. Mashabiki wamemjia juu Rema baada ya clip hiyo kuonesha matukio yanayo husisha na imani za kishetani. Tafadhari tembelea YouTube channel yetu ya Presenterdax kwa taarifa nyingi zaidi.

WEKUNDU WA MSIMBAZI WAOGA MABILIONI YA PILSNER LAGER KWA MIAKA MITATU

Klabu ya Simba Sports Club yenye historia kubwa kuliko klabu chochote katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Katiimeingia mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya Serengeti Breweries kupitia bia yake ya Pilsner Lager. Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema udhamini huu umekuja kuongeza kitu kikubwa sababu uendeshaji wa timu unagharimu kiasi kikubwa cha pesa. Kajula amesema makubaliano haya yatakuwa na faida kwa pande zote huku aliwahakikishia Pilsner kurejea kwa kishindo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. “Tunawashukuru Serengeti kwa kudhamini huu, hamjakosea kutuamiani, mmekuja kwenye klabu sahihi. Tunaamini Muungano huu utakuwa na manufaa makubwa kwa pande zote mbili,” amesema Kajula. Mkurugenzi Mkuu wa Serengeti Breweries, Obina Anyarebenchi amesema makubaliano ya leo lengo lake sio tu kukuza chapa ya Pilsner bali ni kuhakikisha Watanzania wanafurahia bia yao pendwa. “Serengeti tunajivunia mkataba huu, hatujakuja Simba kwa bahati mbaya bali tunaujua ukubwa wa Simba na tunaamini utakuwa na faida kwetu pamoja na wenzetu,” amesema Obina. Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa klabu, Mjumbe wa Bodi Raphael Chegeni amesema Serengeti imewekeza sehemu sahihi na matunda yake wataanza kuyaona kuanzia sasa. “Karibuni sana Serengeti Breweries, mmekuja sehemu sahihi wenye furaha. Simba ni timu kubwa na kwakuanzia Jumapili ya Novemba 5 mnataanza kupata furaha,” amesema Chegeni.

FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE

Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...