Thursday, November 2, 2023
WEKUNDU WA MSIMBAZI WAOGA MABILIONI YA PILSNER LAGER KWA MIAKA MITATU
Klabu ya Simba Sports Club yenye historia kubwa kuliko klabu chochote katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Katiimeingia mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya Serengeti Breweries kupitia bia yake ya Pilsner Lager.
Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema udhamini huu umekuja kuongeza kitu kikubwa sababu uendeshaji wa timu unagharimu kiasi kikubwa cha pesa.
Kajula amesema makubaliano haya yatakuwa na faida kwa pande zote huku aliwahakikishia Pilsner kurejea kwa kishindo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
“Tunawashukuru Serengeti kwa kudhamini huu, hamjakosea kutuamiani, mmekuja kwenye klabu sahihi. Tunaamini Muungano huu utakuwa na manufaa makubwa kwa pande zote mbili,” amesema Kajula.
Mkurugenzi Mkuu wa Serengeti Breweries, Obina Anyarebenchi amesema makubaliano ya leo lengo lake sio tu kukuza chapa ya Pilsner bali ni kuhakikisha Watanzania wanafurahia bia yao pendwa.
“Serengeti tunajivunia mkataba huu, hatujakuja Simba kwa bahati mbaya bali tunaujua ukubwa wa Simba na tunaamini utakuwa na faida kwetu pamoja na wenzetu,” amesema Obina.
Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa klabu, Mjumbe wa Bodi Raphael Chegeni amesema Serengeti imewekeza sehemu sahihi na matunda yake wataanza kuyaona kuanzia sasa.
“Karibuni sana Serengeti Breweries, mmekuja sehemu sahihi wenye furaha. Simba ni timu kubwa na kwakuanzia Jumapili ya Novemba 5 mnataanza kupata furaha,” amesema Chegeni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE
Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...
-
TAARIFA KWA UMMA Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigiz...
-
🟡Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu ya Yanga itasafiri Jumatatu hii November 20, 2023 kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza...

No comments:
Post a Comment