Thursday, November 2, 2023
AHMED ALLY ULIMI UTAKUPONZA SHAURI YAKO JIRANI YAKO ANAKUJA KIMYAKIMYA NA MKUKI WENYE SUMU
"Azam hawezi kutufikia tena, mpinzani aliyebaki ni Yanga ambaye na yeye tunataka kumfunga na kumpita kwa alama sita. Ni mechi ambayo tunaitaka kweli kweli, kuanzia kwa mashabiki, benchi la ufundi, wachezaji na viongozi ndio hata hatulali."
"Tumewekeza zaidi kwenye kuwafurahisha mashabiki wetu, Jumapili ya Novemba 5, 2023 tunataka kuwafurahisha. Na anayeshinda mchezo huo ndio atatawala nchi hadi tukikutana tena."
"Mashabiki wetu tuzingatie misingi ya uungwana na ustaarabu, tujitahidi tushangilia na kutaniana kwa heshima ili kuepusha vurugu. Tuendeleze Utanzania kwa utu na upendo."
"Tumecheza mechi ngumu lakini mechi ya Jumapili ni ngumu kuliko zote hii ni kutokana na utani uliopo pamoja na ubora wa timu yao. Tunaona namna wachezaji wao wanajituma. Mechi yetu dhidi yao ni ngumu kweli kweli, mechi ya kipimo cha mpira wa nchi haiwezi kuwa nyepesi."- Ahmed Ally.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE
Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...
-
TAARIFA KWA UMMA Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigiz...
-
🟡Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu ya Yanga itasafiri Jumatatu hii November 20, 2023 kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza...

No comments:
Post a Comment