Friday, November 17, 2023

SABAYA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA YA RUFAA

Mahakama ya Rufaa imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Kilimanjaro Lengai ole Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura baada ya mahakama hiyo kukubaliana na maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Rufaa hiyo namba 231 ya mwaka 2022 ilikatwa na mwendesha mashtaka wa serikali (DPP) kupinga uamuzi wa awali wa hukumu ya rufaa namba 129 ya mwaka 2021 iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mbele ya Jaji Sedekia Kisanya iliyompa ushindi Sabaya na wenzake baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kufuatia kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021 iliyohusisha wizi na makundi ya unyang’ayi wa kutumia silaha.

No comments:

FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE

Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...