Monday, October 30, 2023
MO DEWJI AUNDA BARAZA LA USHNDI KLABU BINGWA YA AFRIKA NA UBINGWA LIGI YA NBC
Rais wa heshima wa klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ amefanya uteuzi wa wajumbe 21 wa Baraza la Ushauri wa klabu kwa ajili ya maendeleo.
Moja ya majukumu ya Raisi wa heshima ni kuhakikisha Uongozi na Utawala bora unazidi kuboreshwa kila wakati ili kuzidi kusukuma gurudumu la maendeleo ya klabu.
Baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Mo amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Baraza la Ushauri ( Advisory Board) wa klabu.
1. Jaji Thomas Mihayo M/kiti
2. Hassan Dalali-Mjumbe
3. Ismail Aden Rage-Mjumbe
4. Evans Aveva-Mjumbe
5. Faroukh Baghoza
6. Swedi Nkwabi-Mjumbe
7. Azim Dewji-Mjumbe
8. Kassim Dewji-Mjumbe
9. Musleh Al-Ruweh-Mjumbe
10. Mohamed Nassor-Mjumbe
11. Mulamu Ng’ambi-Mjumbe
12. Octavian Mshiu-Mjumbe
13. Prof Mohamed Janabi-Mjumbe
14. Hassan Kipusi-Mjumbe
15. Geofrey Nyange-Mjumbe
16. Gerald Yambi-Mjumbe
17. Moses Kaluwa-Mjumbe
18.Crescentius Magori-Mjumbe
19. Juma Pinto- Mjumbe
20. Mwina Kaduguda-Mjumbe
21. Idd Kajuna-Mjumbe
Kazi kubwa ya Baraza hili itakuwa ni kuishauri Bodi juu ya maendeleo ya klabu Uongozi na Utawala bora.
MKURUGENZI WA SHERIA WA YANGA AMLILIA SHABIKI WAO ALIYEADABISHWA KWA KIPIGO DHIDI YA MASHABIKI WA MNYAMA
Mkurugenzi wa sheria wa Yanga amesema kesho klabu ya Yanga itawasilisha rasmi malalamiko yake kwenye mamlaka juu ya kitendo cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga jana kwa Mkapa.
"Mpira ni upendo, kwa kitendo hiki cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga kiasi hiki sio utu kabisa, hakuna sababu ya msingi kumshambulia mtu kiasi hiki. Labda niwakumbushe washamba wote walioshiriki unyama huu, Yanga na Simba ni Watani wa jadi sio maadui"
"Isije kufika siku hatuwezi kukaa kwa pamoja kama ndugu kwa sababu ya UPUMBAVU kama huu. Naiomba bodi ya ligi @tplboard, TFF @tanfootball na Polisi @policetanzania wachunguze suala hili na hatua kali zichukuliwe"
"Klabu itawasilisha malalamiko yake rasmi kesho na tutaomba hatua kali zichukuliwe kwa huu unyama.. Shame on you all who're involved in this incident"
"Mwenye kumjua na kuwa na mawasiliano ya huyu (Shabiki wa Yanga aliyepigwa na mashabiki wa Simba) anitumie tafadhali"
Licha ya Mkurugenzi huyo kulaani tukio hilo lakini baadhi ya wadau wa Soka wamemshauri kabla ya kutoa tamko alitakiwa kutambua Kiini cha kupigwa dhidi y mashabiki wa timu hiyo ambao hawana historia ya matukio kama hayo tofauti na mashabiki wa Yanga ambao walishamchania mshabiki wa soka Moshi na kuichoma moto.lakini pia mji kasoro bahari Morogoro sambamba na kumpiga shabiki wa Coastal Union jijini Arusha baada kumalizika kwa mikwaju kwenye fainali za FA
AMINI USIAMINI HUYU NI SARAFINA MWIGZAJI MAARUFU ALIETIKISA BONGO
Picha mbili tofauti (zamani na sasa) za Leleti Khumalo mwigizaji toka Afrika Kusini, alizaliwa tarehe 30 Machi 1970 kwa sasa ana umri wa miaka 53. Wengi tunamfahamu kwa jina la Sarafina kutokana na movie maarufu aliyoshiriki ya enzi za ubaguzi wa rangi iliyoitwa SARAFINA!
Unakumbuka nini kuhusiana na movie ya Sarafina? Mimi kuna baadhi ya matukio yalinitoa machozi na kunifanya niwachukie sana wabaguzi wote wa rangi
Two different photos (past and present) of Leleti Khumalo, an actress from South Africa, she was born on March 30, 1970 and is currently 53 years old.
What do you remember about Sarafina's movie? There are some events that brought tears to my eyes and made me hate all the racists
Sunday, October 29, 2023
HARMONIZE APANIA KUWAPAGAWISHA WAKENYA
Harmonize anapomalizia tamasha zake Uganda, ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa atakuwa Nairobi, Kenya tarehe 4.
Harmonize anatarajiwa kufanya ziara zake za muziki kwenye baadhi ya nchi za Afrika mwezi huu ukiisha na Novemba. Amemaliza Uganda anatarajiwa Kenya na nchi zingine Afrika.
As the musician Harmonize finishes his concerts in Uganda, he has written through his Facebook page that he will be in Nairobi, Kenya on the 4th.
Harmonize is expected to make his music tours in some African countries this month ending in November. He has finished Uganda and is expected in Kenya and other countries in Africa.
Saturday, October 28, 2023
MOSSES PHIRI APEWA RUNGU KUWAUA WAKULIMA WA MPUNGA
Mshambuliajii Moses Phiri leo ana nafasi kubwa ya kuanza kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 1 usiku
Jana katika Mkutano na Wanahabari, Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira alidokeza kuwa kuna wachezaji leo atawapa nafasi ya kuanza. Phiri ni miongoni mwa wachezaji ambao pasipo na shaka, anaweza kutumika kwenye mchezo huo
Ukiacha maoni ya Wanasimba na wale wanaohoji kwa nini Phiri hapewi dakika nyingi za kucheza, katika dakika hizo chache, Phiri ameonyesha kuwa na ufanisi kuliko hata wale wanaoanza
Mijadala imekuwa mingi, leo huenda Wanamsimbazi wakafurahi kwa kumuona Mzambia huyo akianza. Wachezaji wengine ambao wanaweza kutumika leo ni pamoja na Luis Miquissone na Shabani Iddi Chilunda ambaye amekuwa akifanya vizuri katika mechi za kirafiki
**************
Subscribe to:
Comments (Atom)
FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE
Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...
-
TAARIFA KWA UMMA Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigiz...
-
🟡Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu ya Yanga itasafiri Jumatatu hii November 20, 2023 kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza...






