Monday, October 30, 2023
MKURUGENZI WA SHERIA WA YANGA AMLILIA SHABIKI WAO ALIYEADABISHWA KWA KIPIGO DHIDI YA MASHABIKI WA MNYAMA
Mkurugenzi wa sheria wa Yanga amesema kesho klabu ya Yanga itawasilisha rasmi malalamiko yake kwenye mamlaka juu ya kitendo cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga jana kwa Mkapa.
"Mpira ni upendo, kwa kitendo hiki cha mashabiki wa Simba kumpiga shabiki wa Yanga kiasi hiki sio utu kabisa, hakuna sababu ya msingi kumshambulia mtu kiasi hiki. Labda niwakumbushe washamba wote walioshiriki unyama huu, Yanga na Simba ni Watani wa jadi sio maadui"
"Isije kufika siku hatuwezi kukaa kwa pamoja kama ndugu kwa sababu ya UPUMBAVU kama huu. Naiomba bodi ya ligi @tplboard, TFF @tanfootball na Polisi @policetanzania wachunguze suala hili na hatua kali zichukuliwe"
"Klabu itawasilisha malalamiko yake rasmi kesho na tutaomba hatua kali zichukuliwe kwa huu unyama.. Shame on you all who're involved in this incident"
"Mwenye kumjua na kuwa na mawasiliano ya huyu (Shabiki wa Yanga aliyepigwa na mashabiki wa Simba) anitumie tafadhali"
Licha ya Mkurugenzi huyo kulaani tukio hilo lakini baadhi ya wadau wa Soka wamemshauri kabla ya kutoa tamko alitakiwa kutambua Kiini cha kupigwa dhidi y mashabiki wa timu hiyo ambao hawana historia ya matukio kama hayo tofauti na mashabiki wa Yanga ambao walishamchania mshabiki wa soka Moshi na kuichoma moto.lakini pia mji kasoro bahari Morogoro sambamba na kumpiga shabiki wa Coastal Union jijini Arusha baada kumalizika kwa mikwaju kwenye fainali za FA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE
Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...
-
TAARIFA KWA UMMA Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigiz...
-
🟡Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu ya Yanga itasafiri Jumatatu hii November 20, 2023 kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza...

No comments:
Post a Comment