Monday, November 13, 2023
JE KOCHA MPYA WA SIMBA NI HUYU BENCHIKHA MBADALA WA ROBERTINOH?
Klabu ya Simba inatajwa kwamba imeanza mazungumzo na Kocha Abdelhak Benchikha ili aweze kuja kuifundisha timu hiyo, mjadala mkubwa hapa ni mshahara wa Kocha huyu ambaye amefanikiwa kubeba makombe mawili makubwa Afrika, Kombe la Shirikisho Afrika na ubingwa wa Super Cup
Kwa mujibu wa tovuti ya 'Transfer Market' Kocha huyu mpaka anaondoka RS Berkane ambayo aliipa ubingwa wa CAFCC 2022 alikuwa akilipwa mshahara wa Tsh.Milioni 53 kwa Mwezi.
Akaenda kujiunga na USM Algers ambao nao aliwapa ubingwa CAFCC 2023 na ubingwa wa Super Cup, mpaka anachana na miamba hiyo ya Algeria alikuwa akilipwa mshahara unaofika hadi kufikia Tsh Milioni 80+
Kiufupi Kocha Benchikha ni mwalimu mwenye mafanikio makubwa kwa soka la Afrika ila pia ana thamani kubwa sokoni.Kama Simba SC wakiweza kumchukua Kocha huyu basi hapo ndo tutasema "Mkubwa hufanya mambo makubwa"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE
Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...
-
TAARIFA KWA UMMA Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigiz...
-
🟡Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu ya Yanga itasafiri Jumatatu hii November 20, 2023 kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza...

No comments:
Post a Comment