Tuesday, October 24, 2023

TUPO TAYARI KUMALIZIA KAZI TULIYOIANZA KWA MKAPA JAPOKUWA AL AHLY NI WAGUMU KWAO-ROBERTINHO

Kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Cairo International leo saa 11 jioni kuikabili Al Ahly katika mchezo wa marudiano wa African Football League Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 20 tulitoka sare ya mabao 2-2. Tunahitaji kushinda mchezo huu ili kutinga nusu fainali ya michuano hii ingawa tunajua haitakuwa kazi rahisi kutokana na ubora wa Al Ahly hasa wakiwa kwao. Robertinho kuja na mbinu tofauti….. Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa atakuja tofauti kulinganisha na tulivyocheza mchezo kwanza jijini Dar es Salaam juzi. Robertinho amesema anategemea pia kufanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji ambao wataendana na mpango wa mechi ya leo. “Mchezo uliopita tulicheza vizuri zaidi kipindi cha pili, nataka tuanze hivyo leo lakini tutakuwa tofauti kidogo kuanzia kwenye upangaji wa timu.” “Pamoja nakuwa tunaiheshimu Al Ahly lakini tumekuja Misri kwa lengo la kupambana tushinde mchezo na tufuzu nusu fainali,” amesema Robertinho. Wachezaji hawajakata tamaa….. Pamoja na kutoka sare ya mabao 2-2 nyumbani wachezaji hawajakata tamaa na wanaamini wanaweza kufanya maajabu ugenini. Kiungo mshambuliaji, Willy Essomba Onana amesema dakika 90 za leo tutazipambani kuhakikisha tunapata matokeo chanya. “Kwenye mpira hakuna kisichowezekana, hata sisi tunaweza kupata mabao mawili kwao, kikubwa wachezaji tupo tayari kupambana,” amesema Onana.

No comments:

FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE

Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...