Saturday, October 21, 2023
Motsepe: AFL imekuja kuongeza uchumi wa klabu
Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Patrick Motsepe amesema lengo la michuano ya African Football League (AFL) ni kuzisaidia klabu za Afrika kiuchumi.
Motsepe amesema timu zinazoshiriki michuano hiyo zinapatiwa kiasi kikubwa cha pesa na zile zinazofanya vizuri zaidi inakuwa kubwa zinaweza kuisaidia kufanya vitu vikubwa zaidi.
Motsepe ameongeza kuwa AFL haitaiua michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kama wengi wanavyodhani badala yake imeanzisha ili kuziongezea klabu uwezo wa kiuchumi.
“Moja ya malengo ya AFL ni kuzisaidia klabu kiuchumi sababu tunalipa kiasi kikubwa, mipango yetu ni kuzifanya klabu za Afrika zijiendeshe kisasa.”
“Idadi kubwa ya wachezaji kutoka Afrika wanatamani kucheza soka barani Ulaya sababu ya malipo mazuri nasi tunataka Afrika tufike kwenye hatua hiyo,” amesema Motsepe.
Motsepe amethibitisha mwakani michuano ya African Football itashirikisha timu 24 badala ya nane ambazo zitashiriki msimu huu.
Friday, October 20, 2023
MWANAMKE BIKIRA WA MIAKA 70 ANATAFUTA MCHUMBAHUKO DRC-HAJAWAHI KUFANYA MAPENZI
Mwanamke bikira ni vigumu kupata katika ulimwengu wa kisasa. Aliphosin Tabarwa, bikira mwenye umri wa miaka 70 kutoka DRC, alisema kuwa yeye ni Bikira ambar hajawahi kutenda tendo la ngono. Hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume. Tabarwa alidai katika mahojiano na chombo cha habari cha Afrimax English kuwa alitoa kila kitu na sio kuhongwa kama wengine ili kujikimu bali alisimama kidete kuwatunza wadogo zake. Aliamua kuachana na anasa za dunia ili aweze kuwalea ndugu zake na kuhakikisha wote wanamaliza elimu ya sekondari. Kwa kuwa aliepuka wanaume na kwa ujumla kukataa kwake hata walipojaribu kumkaribia, hajawa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume kwa miaka 70 iliyopita. Bikira huyo mwenye umri wa miaka 70 pia alikiri kwamba, wakati wenzake wote wa umri wake wameolewa na wana familia, yeye ana ndugu zake tu,ambao nao walioa na kuolewa na mpaka sasa anishi katika mazingira yenye furaha. Usiwe kama Tabarwa wewe, pata mpenzi huyo ameamua kuwa hivyo japokuwa hakuna aliyemchunguza kubaini kama kweli hajawahi....anatafuta mwenza sasa kama vipi unaweza kumtafuta ukajipatia mke swaafi.
Subscribe to:
Comments (Atom)
FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE
Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...
-
TAARIFA KWA UMMA Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigiz...
-
🟡Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu ya Yanga itasafiri Jumatatu hii November 20, 2023 kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza...






