Friday, November 24, 2023
MNORWAY APIGIWA UPATU KUJA KUMRITHI SAMATTA KULE STARS
Kwa sasa stori kubwa mjini Twitter (X) ni Kampeni ya kushinikiza mamlaka husika kumshawishi Mshambuliaji wa Bodø/Glimt, Amahl William D'vaz Pellegrino aje kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania.
🌍Mshambuliaji huyo mzaliwa wa jijini Drammen nchini Norway na wazazi wenye asili ya Tanzania amekuwa tegemeo kunako klabu hiyo ya Norway ambapi tangu amejiunga nao mwaka 2021 amecheza michezo 69 na kufanikiwa kufunga mabao 54.
🌍Licha ya Amhl kuwa na umri wa miaka 33 kwa sasa wanaharakati hao mjini X wanaamini kuwa umri ni namba tu na kijana anastahili kuja kuipa nguvu timu ya taifa lake la asili ikiwa zimesalia siku chache kabla ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika na wakati huu ambapo mamlaka zinajitahidi kuhakikisha wale wote wenye chembechembe za taifa la Tanzania wanakuja kuongeza nguvu kwenye timu ya taifa ya Tanzania.
🌍Kampeni hii imeonekana kuungwa mkono na watu wa kutoka nyanja mbalimbali kama vile waandishi wa habari ,wanasiasa na wengineo ambao wanaamini ongezeko la wachezaji wanaocheza maeneo mbalimbali duniani wataongeza na kuleta mafanikio kwa timu ya taifa. See less
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
FISTON MAYELE ASHINDWA KUTETEMA KWA PERCY TAU WA AL AHLY,CAF YAMUONA NI BORA KULIKO MAYELE
Mchezaji machachari wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na klabu ya Al Ahly Percy Tau amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi za Ndani Barani...
-
TAARIFA KWA UMMA Kampuni ya Azam Media Ltd, imebaini vipande vya picha jongefu vinavyosambaa kupitia mitandao ya kijamii vikimuonesha mwigiz...
-
🟡Taarifa za kuaminika ni kuwa Klabu ya Yanga itasafiri Jumatatu hii November 20, 2023 kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza...

No comments:
Post a Comment